NDOA YAVUNJIKA, KISA MWANAMKE AMEGOMA KUJIBADILISHA ILI AFANANE NA KIM KADARSHIAN.

Admin Updates10 years ago4 Views



Dunia na vioja vingine 2014, eti unaweza kumuacha mpenzi wako kwa kuwa hafanini na staa fulani ambaye wewe unampenda?
Mwanamke
mmoja ambaye jinalake ni Rahma, kutoka Cairo, Misri, amedai talaka kwa
mumewe kwa kuwa amekuwa si mwaminifu, amekuwa akimsaliti mara kwa mara
kutokana na kile ambacho mwanamke huyo amekisema eti mumewe anataka mke
wake afanane na Kim Kadarshian au muigizaji Haifa Wehbe.

Mara
kadhaa mume wa mwanamke huyo amekuwa akimtaka avae na kutengeneza nywele
zake ili afananena mmoja ya mastaa hao, alikataa, amesema anatazama
mambo mengine ya msingi kuyafanya ikiwemo kumlea mtoto wake wa mwaka
mmoja, hivyo asingeweza na hili la kujitengeneza ili afanane na mastaa
hao ambao yeye aliwaita midoli wa kwenye TV!

Kim Kadarshian

Haifa Wehbe, Mwanamitindo, mwanamuziki na muigizaji kutoka Lebanon.

Kwa
kuwa dini ya mwanamke huyo inaongozwa na Sheria ya Shariah ambayo
inaruhusu mwanamke kuachika na mahari iliyotolewa kurudishwa, mwanamke
alifanya maombi ya kudai talaka ili aendelee na maisha yake mengine.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.