UKWELI KUHUSU KUKOSANA KWA AKI NA UKWA UKO HAPA WENYEWE WAFUNGUKA

Admin Updates10 years ago6 Views


Aki
na Ukwa ni marafiki wawili wanaokonga nyoyo za watazamaji wa filamu
nchini na Nigeria na Afrika kwa ujumla. Wawili hawa wana sifa ya ufupi
huku pia watu wengi wamekuwa wakidhania ni ndugu au mapacha. Kwa mujibu
wa Aki, waigizaji hao hawana undugu wao ni marafiki wazuri sana.Marafiki
hawa wamekuwa wakiishi pamoja kwa muda mrefu ingawa siku za hivi
karibuni wameoneka kila mmoja akiishi kwenye makazi yake, kitu ambacho
watu wengi walitafsiri kuwa huenda wametengana na kwamba inawezekana
kuna ugomvi kati yao.
Kutokana na uvumi huo, Aki alijitokeza na kuzungumza na gazeti la Tribune kutoa maelezo ya kinachoendelea;
Aki ambaye jina lake halisi ni Chinudu Ikedieze anasema:
Hakuna
ugomvi kati yetu suala ni kwamba sehemu tuliyokuwa tunaishi mwenye
nyumba aliichukua hivyo ikatubidi tutoke. Ukweli ni kwamba hatuwezi
kuishi pamoja maisha yetu yote.
Sisi ni watu wazima sasa na siku moja
tunaweza kuwa na familia. Sisi sio mapacha, mimi natokea jimbo la ABIA
na yeye anatokea Jimbo la IMO, ni kwamba sisi ni marafiki wazuri. Si
vibaya kila mtu akienda upande wake ingawa hatukai mbali.”
Alipoulizwa kwamba umaarufu wake ulikuja baada ya kukutana na Pawpaw (Ukwa) akajibu:
Haikuwa
hivyo, nimeanza kuigiza tangia mwaka 1998 wakati huo bado nasoma chuo
kikuu na nikaweza kufanya kazi miaka ya 1999 na 2000. Kwahiyo nimekuwepo
kabla ya Ukwa ambaye alianza kuigiza mwaka 2001 na hakuwa maarufu. Kwa
muujiza wa Mungu tukajikuta pamoja na kufanya filamu ambayo
tulishirikishwa na ambayo ikatupa utofauti mkubwa kwa sababu ya kimo
chetu.
Ninaamini kwamba sisi sio watu pekee wafupi ila ni sanaa
iliyopo ndani yetu ambayo muunganiko wake ukaipa sanaa ya filamu sura
tofauti. Kumbuka hatukuanza kwa kuchekesha ingawa nilipokuwa shule ya
sekondari rafiki zangu walinijua kwa uchekeshaji.
Kila jambo
lililotokea maishani kwangu ni kwa sababu, na ninaamini watu wanatakiwa
kujua historia yangu na maisha yangu nje ya uigizaji. Ninachoweza kusema
kuja kwetu pamoja na Ukwa kulileta hamasa katika filamu za
uchekeshaji.”
Kuhusu namna alivyoanza kuigiza, muigizaji huyo alisema:
Nimesoma
taaluma ya mambo ya habari katika chuo kimoja huko Enugu (taasisi ya
Uongozi na teknolojia). Ninakumbuka nikiwa sekondari nilikuwa kwenye
kikundi cha uigizaji na vile vile nilikuwa naigiza kanisani. Ninaweza
kusema hayo yote yaliijenga taaluma yangu ya uigizaji ingawa nilikuwa
sijioni kama mwigizaji.
Mwaka 2004 niliweza kuhudhuria tamasha la
filamu New York Marekani kwa wiki nane mfululizo, elimu ndogo
niliyoipata huko ilinisaidia , ingawa kuna changamoto nyingi. Mara
nyingi kukatishwa tamaa hasa tunapoenda kwenye kuchaguliwa ilikuwa kazi
sana lakini sikukata tamaa mwishowe nikaweza kufanikiwa.”

Aki na mke wake
Vile
vile aliulizwa kama watu walishaweza kumchukulia kama mtoto na kusema:
Wote ni binadamu kila mtu akiniona kwa mara ya kwanza anafikiri ni mtoto
na nikiongea fikra inabadilika na kuelewa kuwa mimi sio mtoto kama
wanavyodhani. Sikujiumba mwenyewe na siwezi kujibadilisha na wala hakuna
kitu ninaweza kufanya kuongeza urefu. Nimegundua ninaishi kwenye
ulimwengu ambao watu walichukulia mambo wanavyodhani, hivyo watu wazima
wanaweza kukutana nami na wakafanya vitu vya ajabu, wengine hunidhihaki
na wengine kunicheka. Watu wengi wanashindwa kuelewa Aki wanayemwona
kwenye televisheni au filamu ni tofauti sana na Chinedu Ikedieze.”
Alipoulizwa
kuhusu ndoa kama imeondoa yeye kufurahia maisha alisema, maisha ya
ukapera ni tofauti sana na ndoa. Kwenye ndoa unahitaji kumheshimu mwenza
wako na unatakiwa kufanya mambo kulingana na mahusiano yenu hivyo kuna
baadhi ya vitu itakulazimu kuviangalia kwa upya. Alisema pia anafurahia
ndoa yake na anamshukuru Mungu kwa hilo ingawa anasema ni majukumu mapya
tofauti na unapokuwa hujaoa.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.