WEMA, WOLPER WALEWA CHAKARI!,KISA MSONGO WA MAWAZO KIKO HAPA…ANGALIA WALIVYOKUWA JANA USIKU

Admin Updates10 years ago5 Views

Mastaa
warembo kutoka Bongo Movies,  Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper
Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa
kwamba wana msongo wa mawazo.

Wema, Wolper Walewa Chakari!,Kisa Msongo wa Mawazo



Gazeti
la Risasi la jana, limeripoti kuwa tukio hilo lilijiri hivi karibuni,
usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya
Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya
jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na
mastaa kibao.

Katika
pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu
waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.



Tofauti
na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali
hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo
liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao
walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na
wastaarabu kupita maelezo.



Baada
ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha kukata mauno
kabla ya Wolper kuzimika kufuatia kuzidiwa na ‘kinywaji’.Kwa upande wake
Wema alimpiga vibao mwanaume shoga aliyetajwa kwa jina moja la Danny
baada ya kutibuana kabla ya watu kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka
mahali hapo, ilidaiwa kwamba Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye
gari kwani alikuwa hajiwezi.



Uchunguzi
wa gazeti hilo umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa mawazo hivyo
wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.



Habari
za ndani zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo na njia pekee
ambayo huitumia ni kujipooza kwa pombe kali.

“Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).



Ilisemekana
kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye nyumba ambayo
Wema alikuwa na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala la jamaa huyo
kutanua na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ limekuwa
likimpa wakati mgumu mwanadada huyo.



Habari
zilieleza kuwa, jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo ni suala
la kukosa mtoto kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua yeye ni
mgumba.Pia ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa kufilisika
kwani kwa sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa na
heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza mawazo
ni kunywa pombe.



Kwa
upande wake Wolper uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda fedha
hivyo kukosa tenda za kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za Kibongo
kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye anataka
kuishi maisha ya kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na mshiko.



Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa.
-bongomovies
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.