HATIMAYE 18 WAPITA MCHUJO WA KWANZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

Admin Updates10 years ago4 Views

Baadhi ya Majaji wakijiandaa kutangaza Rasmi Matokeo ya washiriki 18 walioingia katia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Kutoka kulia ni Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
 Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,
Eluka
Kibona akiwakaribisha majaji kutangaza matokeo ya washindi
 Zephaniah Muggitu a ambaye pia alikuwa ni Jaji  Akieleza kwa ujumla Jinsi mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyokuwa
 Bw.
Jairos Mahenge ambaye Pia alikuwa ni Mmoja wa Majaji akizungumzia kwa
ufupi changamoto walizokutana nazo wakati wa Mchakato mzima wa kuhakiki
fomu za kuwapata washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
 Ofisa
Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo
mafupi ya Jinsi watakavyo watembelea washindi 18 katika maeneo walipo
ili kuona shughuri zao na baadae kuwapata washiriki 15 ambao ndio
wataingia katika mshike mshike wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015
Dora

Myinga ambaye pia alikuwa ni jaji akiwataja washindi 18 walioingia
katika shindano la safari ya kumpata  Mama shujaa wa Chakula

Baadhi ya majaji wakiwa wanaendelea na kazi wakati wa kuwatangaza washindi walioingia kuanza safari ya kumsaka Mama Shujaa wa Chakula 2015
*****
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu
za washiriki wa shindano la mama shujaa wa chakula 2015 kukamilika,
takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita
katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano
hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata
mshindi.

akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa
majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki,
Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao
ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.

Jaji
huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi
ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao
ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za
juu kutoka mikoa tofautitofauti.
Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania 
Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote  watatembelewa
maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae
kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.

Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie  L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel
Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel
Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang  Manyara,  Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva
Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani 
Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida,
Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini,
Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera 
Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48)  Kilombero Morogoro, Stella Fabian  Masulya (42) Ukerewe Mwanza,  Regina Kapili Stephano (19)  Mpanda  Katavi, Rehema Daniel  Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.
WEKEZA KWA WAKULIMA WANAWAKE WADOGO WADOGO INALIPA 

 
 
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.