BATULI WA BONGO MUVIE ANASWA CHUMBANI NA MWANAUME WAKIFANYA YAO

Admin Updates9 years ago6 Views

Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ katika mahaba mazito na mchekeshaji Stan Bakora.
DAH! Wakati mashabiki wake wakiamini si mtu wa ‘kurukaruka’ kivile, muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ amekwaa aibu baada ya picha zake zikimuonesha akiwa kimahaba chumbani na mchekeshaji Stan Bakora kuvuja, Ijumaalinakupa mchapo kamili.
TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kilichovujisha ubuyu huo kilieleza kuwa, kina picha zinazomuonesha Batuli akiwa kimahaba na Stan bila kujua walizipiga kwa ajili gani.

“Nina picha za Batuli akiwa na kanga moja, anaonekana yuko na Stan Bakora ‘on bed’, sijajua wamezipiga za nini ila ukiziona nadhani unaweza kuzifanyia kazi,” kilidai chanzo hicho.

Ijumaalazinasa

Baada ya picha hizo ambazo kimsingi ziko kinyume kabisa na maadili ya Kitanzania (kwenye filamu haziwezi kuonekana na hata kwenye gazeti haziwezi kuchapishwa) kutua kwenye dawati la gazeti hili, jitihada za kupata undani wake zilianza kwa kuwatafuta wahusika.

Bofya hapa kumsikia Batuli

Paparazi: Mambo Batuli?

Batuli: Safi vipi kuna usalama huko maana asubuhi sana hii?

Paparazi: Huku usalama upo isipokuwa kuna picha uko na Stan Bakora, vipi ndiyo umeamua kujiweka mazima?

Batuli: Mmmh… Tafadhali hizo picha kuna ‘project’ nimefanya na Stan Bakora kwa hiyo naomba zisitumike kunichafua maana mimi kuna ishu muhimu sana natarajia kuifanya kipindi hiki cha uchaguzi.

Paparazi: Oke mimi nilitaka kujua hilo tu maana nimeona jinsi picha zilivyo za mahaba nikaona ni vyema kujua mantiki ya picha hizo kutoka kwako?

Batuli: Ujue hizo picha najua atakuwa kakupatia Mkude Simba na lengo lake ni kufanya promo ya muvi yake, mimi sitapenda kwa kipindi hiki nichafuke, please naomba usizitumie.

Paparazi: Hajanipa Mkude Simba. Kikubwa nilitaka kujua hizo picha umezipigia wapi?

Batuli: Nimekwambia ni filamu na sitaki zitumike kunichafua.

Paparazi: Hiyo filamu mlishuti wapi?

Batuli: Morogoro ila mimi sikutaka kukaa kambini, nilienda kushuti na kurudi zangu Dar.

Paparazi: Nakushukuru sana.

Alipotafutwa Stan Bakora kuhusiana na picha hizo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Batuli, alisema:

“Ni muvi kaka, katika hali ya kuuvaa uhalisia ndiyo tulipiga kimahaba zaidi lakini sina uhusiano wowote na Batuli.”

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.