Chuchu akolea kwa Ray aapa kuolewa naye

9 years ago99 Views

Stori: Imelda Mtema

LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.

Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na Chuchu hans

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana mapenzi ya dhati kwake.

Vincent Kigosi ‘Ray’

“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,” alisema.

Chuchu Hans

Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani nalo,” alisema.

GPL

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.