Msadizi wa Jeshi la Zimamoto Castory Willa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kigamboni linaendealea kutoa mafunzo kwa wananchi na wafanyakazi wa makampuni na taasisi mbalimbali ili kuadhimisha vema mwaka mpya pasipo matukio na ajali za moto.
Akitoa Maelezo kwa wafanyakazi kampuni ya TIPPER, Mkaguzi Msadizi wa Jeshi la Zimamoto Castory Willa amewaeleza namna mbalimbali za kupambana na moto kwa kutumia vifaa vya Zimamoto (Fire extinguisher).

Akijibu maswali Afande Willa alieleza kuwa katika baadhi ya matukio jeshi la zimamoto wanachelewa kufika eneo la Tukio (Tukio la Dampo kigamboni tar 27/12/2016) kutokana na umbali kutokea magari yalipo. Kwa sasa wanategemea Magari ya Zimamoto kutoka Wilaya ya Ilala, Temeke, na Kinondoni. Pia wanachelewa kutokana na miundombinu na foleni barabarani.
Pia ameeleza kuwa wananchi wengi huwa hawapigi namba za dharula (114) kwani hawaijui jambo linalowafanya wasipate taarifa kwa wakati.
Kuhusu Maji katika magari ya kuzimia moto amesema huwa wanabeba maji ya kutosha ila kinachotokea ni kwamba tenki moja la maji huweza kuisha ndani ya dadika 3 hadi 10 kutokana na kasi ya maji yanapotoka na hivyo kuisha haraka wakati mwingine kabla moto haujazimwa kabisa.
Amesema mkesha wa Mwaka Mpya kutakuwa na Gari la Zimamoto likiwa tiyari ili kukabiliana na dharula yoyote itakayojitokeza kwa siku hiyo ili kuiweka wilaya ya Kigamboni katika hali ya usalama.
Ameonya kuwa, yoyote atakae husika na KUCHOMA moto matairi au vitu vingine ambavyo ni hatarishi kwa usalama atachukuliwa hatua kali za kisheria, hivyo yoyote mwenye mpango wa kufanya hivyo aache.
Afande Willa amewaomba na kuwahamasisha wananchi kuhudhuria mafunzo ya Zimamoto yatakayokuwa yakitolewa kwa nyakati tofauti na kuwa wataanza na Kata ya Kigamboni tar 31/12/2016 na Kata nyingine zitafuata. Hii ni kujiimarisha kukabiliana na matukio ya moto.