Baadhi ya wafanyabiashara wa maziwa wameiomba serikali kupunguza kodi za tozo mbalimbali zinazotozwa katika bidhaa hizo ,ili kuwezesha wananchi wa kufungua viwanda vya kusindika maziwa hapa nchini .
Akizungumza na Waandishi wa habari katika maadhimisho ya Wiki ya unywaji maziwa duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa,Meneja wa mauzo wa kampuni ya Cowbell Vitus Mpanda Alisema kuwa kodi nyingi zilizopo katika nchi yetu zinawanyima wafanyabiashara wengi kufungu viwanda vya maziwa
Alibainisha Kuwa gharama zimekuwa kubwa mno katika biashara hii ya maziwa, kwani tozo ni nyingi mno hali inayosababisha baadhi ya viwanda vya maziwa kufungwa.
Aidha aliomba serikali kuunganisha kodi ya TBS pamoja na TFDA kwani vitengo hivi vinafanana na tozo yake ni kubwa mno na pia mpaka upate vibali vyake ni kazi mno
“gharama za kusindika maziwa pia hapa nchini ni kubwa mno kuliko nchi za wenzetu, kwani Nchi za wenzetu wanasindika kwa bei ya chini hivyo mfanyabiashara anaona bora akasindike nje ndipo aje auze hapa nchini “alisema Isaya Mbindi
Alisema kuwa mbali na hapo wafugaji Wengi wanapenda kufuga lakini kutokana na garama za ufugaji zilivyo juu wanashidwa kufuga.
Alisema kuwa mbali na garama kubwa pia aliomba serikali kuwapatia elimu zaidi wafugaji ili waweze kufuga kisasa na kufanya ufugaji bora ili waweze kupata maziwa bora
Baadhi ya mabanda yaliopo kwenye maonesho ya wiki unywaji maziwa duniani ambapo kitaifa yanafanyika jijini Arusha katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid 