WAFANYABIASHARA WA MAZIWA WAIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA KODI ZA TOZO ZA MAZIWA

6 years ago75 Views

Na Woinde Shizza, Arusha

Baadhi ya wafanyabiashara wa maziwa wameiomba serikali kupunguza kodi za tozo mbalimbali zinazotozwa  katika  bidhaa hizo ,ili kuwezesha wananchi wa  kufungua viwanda vya kusindika maziwa hapa nchini . 

Akizungumza na Waandishi wa habari katika maadhimisho ya Wiki ya unywaji maziwa duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa,Meneja wa mauzo wa kampuni ya Cowbell Vitus Mpanda Alisema kuwa kodi nyingi zilizopo katika nchi yetu zinawanyima wafanyabiashara wengi kufungu viwanda vya maziwa 

Alibainisha Kuwa gharama zimekuwa kubwa mno katika biashara hii ya maziwa, kwani tozo  ni nyingi mno hali inayosababisha baadhi ya viwanda vya maziwa kufungwa. 

Aidha aliomba serikali kuunganisha kodi ya TBS pamoja na TFDA kwani vitengo hivi vinafanana na tozo yake ni kubwa mno na pia mpaka upate vibali vyake ni kazi mno 

“gharama za kusindika maziwa pia hapa nchini ni kubwa mno kuliko nchi za wenzetu, kwani  Nchi za wenzetu wanasindika kwa bei ya chini hivyo mfanyabiashara anaona bora akasindike nje ndipo aje  auze hapa nchini “alisema Isaya Mbindi 
Alisema kuwa mbali na hapo wafugaji Wengi wanapenda kufuga lakini kutokana na garama  za ufugaji zilivyo juu wanashidwa kufuga. 

Alisema kuwa mbali na garama kubwa pia aliomba serikali kuwapatia elimu zaidi wafugaji ili waweze kufuga kisasa na kufanya ufugaji bora ili waweze kupata maziwa bora
 Baadhi ya mabanda yaliopo kwenye maonesho ya wiki unywaji  maziwa duniani ambapo kitaifa yanafanyika jijini Arusha katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid 

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2XeHAOz
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.