Pep Guardiaola Afunguka : Nastahili Kufukuzwa Man City

Admin Updates6 months ago6 Views

Kocha wa Manchester City Josep ‘Pep’ Guardiaola (53), amesema kuwa huenda anastahili kufukuzwa kutokana na muendelezo wa matokeo mabovu wanayoyapata, baada ya jana kushuhudia timu yake ikipoteza mchezo wa nne mfululizo katika Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool pale Anfield.
Baada ya mchezo kuwisha Pep alisema: “Najivunia kushinda makombe sita ya Ligi Kuu ya Uingereza na sikutegemea mashabiki wa Liverpool kupiga kelele nifukuzwe, labda nastahili kufukuzwa kwa kweli”.
Pep Guardiaola baada ya mchezo kumalizika alionekana akiwanyooshea vidole sita mashabiki wa Liverpool, ikiwa ni ishara ya mataji ya Ligi Kuu ya Uingereza ambayo ameshinda mpaka Sasa akiwa na Manchester City.
Aidha Pep katika mkutano na wanahabari aliongeza kuwa anaimani kila mtu katika timu yake atarejea katika hali yake ya kawaida, Kwa pamoja watapambana kuelekea mchezo wa Jumatano Desemba nne dhidi ya Nottingham Forest.
Manchester City imeshindwa kupata ushindi katika mechi saba mfululizo, ambapo mchezo wa mwisho kupata ushindi ilikuwa dhidi ya Southampton, Oktoba 26 mwaka huu.

Manchester City baada ya kipigo cha 2-0 hapo jana, wameshuka mpaka nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa na alama 23 baada ya michezo 13 tofauti ya alama 11 na vinara Liverpool. 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.