Kampuni ya kutengeneza Mabasi aina ya Yutong imetoa mafunzo kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji nchini, namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi katika mabasi hayo yanayofanya safari zake mikoani na nje ya nchi ili kuweza kujikinga pindi yanapopata hitilafu na kuwaka moto lengo ikiwa ni kupunguza ajali za moto.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yamefunguliwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi,Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Fikiri Salla huku washiriki hao wakifundishwa nadharia na vitendo katika kudhibiti majanga ya moto na ikiwa pamoja na kuangalia mifumo ya magari hayo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Kamishna Fikiri alisema sasa ni wakati wa sayansi na teknolojia na jeshi halina budi kuanza kujifunza njia mbalimbali za udhibiti wa majanga kwa kutumia teknolojia huku akiishukuru kampuni ya Yutong kwa mafunzo hayo.
“Tunapitia kipindi cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia naamini mafunzo haya yatawawezesha askari wetu kujifunza njia hizo za kisasa sambamba na kuelewa mfumo mzima wa mabasi hayo ambayo yamekua mengi hivi sasa hapa nchini na yakitumika katika usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali” alisema Naibu Kamishna Fikiri
Aidha mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong wakiongozwa na Meneja Huduma wa Kampuni hiyo, Lang Chang Ling,Mtaalamu wa Usalama kwenye gari,Ma Jiong na Mhandisi wa Huduma, Zhao Le Hui
Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili walisema wanaamini baada ya mafunzo kumalizika watakua wamepata elimu ambayo itawaongezea kitu katika shughuli zao za kila siku zinazohusiana na majanga ya moto na uokoaji.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi Naibu Kamishna Fikiri Salla, akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji(hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo ya namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasi aina ya Yutong. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yakiendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mabasi ya Yutong Lang Chang Ling akitoa ufafanuzi jinsi mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasihayo kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma ,leo ambapo mafunzo hayo ya siku mbili yameanza.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2DIGBOn
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








