Meli ya mizigo ya MV Umoja iliyobeba mabehewa ya treni yenye shehena ya mzigo wa Shirika la Programu ya Chakula Duniani (World Food Program-WFP) kutoka Mwanza kwenda Uganda iliwasili bandari ya Portbell, Uganda tarehe 31 Julai 2019.
Katika Halfa ya mapokezi ya meli hiyo, Serikali ya Uganda iliwakilishwa na Waziri wa Nchi-Uchukuzi, Mhe. General Katumba Wamala na kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Dkt. Aziz Mlima alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.
Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam hadi Kampala.
Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa kutumia njia hii wameokoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 2.
Ujumbe uliosafiri na meli ya MV Umoja iliyobeba mabehewa hayo yenye mizigo ya WFP ulijumuisha Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa; Mkurugenzi wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Johnson Kisaka ambao waliambatana na Mkurugenzi wa WFP-Tanzania, Bw. Michael
![]() |
| Meli ya MV. Umoja iliyobeba shehena ya mzigo, mali ya WFP kutoka Dar Es Salaam ikiwasili katika Bandari ya Port Bell jijini Kampala tarehe 31 Julai 2019. |
![]() |
| Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima akitoa neno wakati wa hafla ya mapokezi ya meli ya Mv. Umoja jijini Kampala, Uganda. |
![]() |
| Balozi Mlima akiongea na wanahabari kuhusu zoezi hilo. |
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KacbbO
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33










