Huyu ndio wema ninaye mjua mimi!!
Kwakifupi
mimi binafsi nilimsikia Wema Sepetu kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka
2006 akiwa mshindi wa taji la MISS TANZANIA 2006….(Kama unakumbuka
ushindi wake uliandamwa na kashfa za rushwa za ngono, na fitina
kibao)..Baada ya hapo hakufanya vizuri kwenye mashindaono ya MISS WORLD
ya mwaka huo akiwa kama mshiriki kutoka TANZANIA. (Enzi hizo nahisi
Diamond alikuwa hana hata Simu ya mkononi)
Baada ya hapo
zikafuata kashfa mbalimbali za Ku-DATE na mstaa Kadhaa kuanzia wa
muziki, maigizo, Madingi nk (List ya majina ni ndefu sana itatujazia
page)
Miaka ya hivi karibuni akaibukia Bongo Movie na kuwa muigizaji,
na kacheza filamu kadhaa (Enzi za kila demu mzuri au miss anaingia
kwenye tasnia). Enzi ya ZE GRETI KANUMBA (R I P, bro wewe ndio MUINZIGA
HUKU)….Kama kawa huku nako alifanya vizuri kidogo (kibongo bongo)
FOMEKINGI LONGI STORY SHOTI
Hatimaye akatua kwenye mikono ya Diamond baada ya kuwa na mastaa kadhaa (Daah hapa kuna ka -list tena kabla ya Diamond)
Kwasasa
ni C E O wa kampuni yake ya ENDLESS FAME (kua yake au sio yake hapa sio
Ishu) inayojishughulisha ya maswala ya MOVIES PRODUCTION, NK..Ambayo
aliifungua siku za hivi karibuni. Mwisho kabisa nimeambiwa anakipindi
kwenye TV, sijajua kinaitwaje BUT nasikia anajizungumzia mwenyewe na
maisha yake….akiwa na wale jamaa zake (and of coz bila kumsahau Meneja
wake……hehehehe)
And business as usually, Kila siku yupo kwenye
Media na skendo tofauti tofauti mara kagombana na huyu kisa BWANA, mara
Ndugu wa Diamond hawamtaki…basi ilimladi watu wamsikie tu (Diamond
alishaeleza mara kadhaa kuwa Wema huwa anazipeleka mwenyewe skendo kwa
magazeti ya UDAKU-Nanasikia mwaka huu wamempa na TUZO).
Sasa kwanini nimeuliza:
Kwanza
kabisa ni kweli Story za Wema ndio zinazoongoza kwa kusomwa na wapenda
Udaku watu wa Blogu (Kama mimi), Magazeti ya Udaku, majarida na
Radio,TV watakubaliana namimi kuwa story za huyu MDADA siauza sana
(Kwahiyo zinapendwa)
Kwenye mitandao ya kijamii Wema Sepetu ana
watuwengi zaidi wanao mfuatilia kuzidi mastaa wote wa hapa BONGO:
Tuanze na FESIBUKU ana LIKES zaidi ya LAKI MOJA, TWITA na Followers
zaidi ya ELFU THEMANINI, INSTAGRAM ana Followers zaidi ya LAKI NA
ISHILINI…Hatari Sana…hakuna staa yoyote anamkaribia kwanye hili.
Akounti za TEAM Wema nazo zina watu wakutosha (Kazi yao kubwa ni kusifia na kusafisha hali ya hewa kama Wema amaichafua)
Kwamfano ipo hii inajiita WEMA REPLIES wapo INSTAGRAM (Hawa kutwa wao wema tu)
Sasa facts zipo hivi:Kwenye U-MISS; Hivi Wema anamfikia kweli Nancy Sumari ambaye alitwaa taji la Afrika?
Kwenye Kuigiza; Hivi Wema anauwezo gani wakumzidi Johari au Monalisa?
Kwenye TV: Hivi kipindichake kina ubunifu na mvuto gani? unawza kufananisha na kipindi kama wanawake LIVE,au Mkasi?
Nikweli kwamba Wema hana chakumfanya awe hivi alivyo….Naomba wadau mnisaidie kuniambia
HUYU WEMA NI NANI KUWA USHAWISHI KIASI HICHI?.