Matokeo ya Kidato cha Nne 2019 yaliyotangazwa mnamo tarehe 09, Januari 2019, na Baraza la Mitihani Tanzania, yameendelea kusisimu wadau mbalimbali wa Elimu kufuatia baadhi ya Wahitimu kuonesha maajabu katika ufaulu wao.
Miongoni mwa maajabu na rekodi iliyojitokeza katika matokeo hayo, ni pamoja na waliokuwa Wanafunzi sita wa Shule ya Seminari ya Katoro iliyopo Mkoani Kagera, kufaulu kwa alama nzuri sana katika matokeo ya Mtihani huo wa kuhitimu kidato cha nne mwaka jana.
Hali hiyo imeonekana kuwashangaza walio wengi kwani si jambo rahisi sana Kwa hofu ya mtihani inavyokuwa, lakini watuhumiwa hawa wameweza kufanya vizuri baada ya kuomba nafasi hiyo Kwa mamlaka zinazohusika na kesi yao, mpaka sasa upepelezi wa kesi yao haujakamilika licha ya kuonekana wazi dalili za uonevu kulingana na mlolongo wa kesi yao ulivyo.
Wanafunzi hao ambao mpaka sasa wapo mahabusu Kwa kushikiliwa Kwa Tuhuma za kifo cha Mwanafunzi mwenzao kilichotokea miezi kadhaa iliyopita, wametambulika Kwa majina yao na ufaulu katika mabano kuwa ni Sharifu Amri (Division II.19), Fahad Abdul-Azizi (Division II.21), Hussein Mussa (Division II.21), Sharifu Uledi (Division II.21), Abdallah Ntarambe (Division III.23), na Usama Ramadhani (Division III.25).
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2t7rRab
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33










