NA MWAMVUA MWINYI, Chamakweza
WAKAZI jamii ya Wafugaji wa Kijiji cha Chamakweza Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo Pwani, wameanza ujenzi wa shule ya sekondari ambayo ikikamilika itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule mbalimbali.
Hatua hiyo itahamasisha baadhi ya jamii hiyo wanaoshindwa kusomesha watoto wao na wengine kushindwa kuwapeleka kwenye shule za Moreto na Chalinze ambazo ni za bweni na kutwa.
Wakizungumza kwenye eneo la ujenzi, Michael Kashina,
Lepa Mumbi na Solomon Madongo walisema ,ujenzi huo umeanza kutokana na juhudi za Lekope Langw’esi diwani wa Kata ya Pera, kata ambayo kwa sasa baadhi ya vijiji vyake vilivyokuwa katika kata hiyo vimehamishiwa Kata ya Vigwaza.
Kashina alieleza, katika harakati hizo wametumia shilingi milioni 13 kwa ajili ya kuweka bati kwenye vyumba vitatu na ofisi moja, ili wakipata ridhaa toka halmashauri waanze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani, hatua inayopunguza msongamano katika shule zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.
“Langw’es akishirikiana na viongozi wenzake pamoja na wananchi walikaa kisha kuzungumza na mkazi aliyekuwa ameanza ujenzi wa sekondari binafsi, ambapo aliishia njiani ili awaachie majengo hayo yaliyopo ndani ya eka 50 kisha wampatie eneo mbadala”
Nae Mumbi alisema , miliki wa jengo hilo alilolenga kuwa sekondari ya binafsi, ameshindwa kulimalizia, hatua iliyowalazimu wao kumfuta wakamuomba ili wajenge shule ya Kata, kisha wao kumpatia eneo lingine lenye ukubwa wa eka 50 sawa na hilo.
Diwani Langw’esi aliwashukuru wananchi wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wao kwa kukaa kisha kuibua mradi huo unaolenga kuwaondolea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34aLawI
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







