Kamati ya Ulinzi na usalama kupitia jeshi la polisi mkoa wa Tabora limeahidi Kuongeza nguvu ya Ulinzi na usalama katika Soko kuu la Madini mkoa wa Tabora kwa kutumia mbinu za kiteknolojia na kuimarisha Ushirikiano dhidi ya Wachimbaji wadogo na Serikali lengo ikiwa ni kuhakikisha wauzaji na wanunuzi wa Madini wote wanakuwa na Ulinzi na usalama dhidi ya biashara hiyo
Yamesemwa hayo hii leo mjini Nzega Mkoani Tabora katika Ufunguzi wa soko la Madini ambalo limejengwa kisasa huku likizingatia Weledi wa juu pamoja na kutekeleza agizo la Serikali ya Awamu ya Tano
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Emmanuel Nley amesema biashara hiyo itakuwa safi na salama Kamati ya Ulinzi imejipanga kuimarisha suala hilo kwa vitendo zaidi
“Soko kuu la kununua na kuuza dhahabu litaimarishwa sana kutakuwa na Askari wa aina mbili Askari wanaovaa Uniform watakuwa hapa na Askari wanaovaa kiraia watakuwa hapa katika jengo hili na zitafungwa teknolojia zilizoimatishwa kutakuwa na CCTV Camera na vyombo vya moto kwa hiyo katika jengo hili kutakuwa na Usalama “Amesema Nley
Kwa upande wake katibu Tawala mkoa wa Tabora Robert Makungu amesema soko hilo limezingatia vigezo vya kibiashara kwani huduma za kifedha zinapatika bila usumbufu wowote
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema hatarajii kusikia watu wanatorosha Madini .”Sitaki kusikia mtu anakamatwa kwa kosa la kutorosha Madini atakayekamatwa atachukuliwa hatua za sheria na mtu huyo atakayefanya hivyo ujue hataki maendeleo ya nchi “Amesema Mwanri
Aidha Serikali ya mkoa wa Tabora imeendelea kuwatoa hofu wauzaji na Wafanyabiashara wa kuwauzia Madini katika soko hilo ambapo imesema bei itakuwa ni rafiki na hakutakuwa na ubabaishaji na soko hilo litawasaidia Wafanyabiashara wa Madini kutokwenda nje ya mkoa kuuza madini yao kwani soko hilo limekidhi kila kitu.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2UZg6dO
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







