Muda mfupi kabla ya hapo, milango ya Sistine Chapel ilikuwa imefungwa kwa kauli ya jadi “Extra omnes” yaani, “Wote watoke” ikiashiria mwanzo wa mchakato wa upigaji kura wa siri.
Makardinali 133 wanaendelea na jukumu lao zito la kumchagua Papa wa 267 wa Kanisa Katoliki. Conclave itaendelea kesho asubuhi, saa 4:30 kwa saa za Roma, ambapo makardinali watakusanyika tena kupiga kura mpya. Dunia inaendelea kusubiri kwa hamu dalili ya moshi mweupe ishara ya Papa mpya.