Na Joachim Mushi
MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana uliwasimamisha waandishi wa habari mbalimbali kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano nao, ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Marehemu Dk. Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP ambaye amefariki dunia.
Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga alisema Marehemu Mengi alikuwa mmoja wa wadau wa elimu na amefanya mambo mengi kuchangia mafanikio ya sekta hiyo hivyo wanakila sababu ya kumkumbuka.
“…TEN/MET imeguswa na msiba wa Marehemu Dk. Mengi kwa kuwa alikuwa mdau mzuri katika kuchangia elimu, amefanya mambo mengi kuchangia na kusaidia wahitaji katika elimu…naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka,” aliwaambia wanahabari.
Jana TEN/MET ilikutana na waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar es Salam kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni.
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga akizungumzia maadhimisho hayo alisema mwaka huu yataanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.
“…Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”.
Aidha alisema maadhimisho ya juma la elimu yatazinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleman Jafo mkoani Tanga yatakayofanyika Wilayani Handeni.
“…Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”. Alisema Mratibu huyo.
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto).
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2UZFTm3
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 - Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33