Na. Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platnum amewaasa wasanii kutumia Sanaa yao kuongeza pato la taifa.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam wakati akitangaza rasmi ujio wa Tamasha la wasafi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam amesema kwa mwaka huu imekua neema kwa wasanii wasanaa mbalimbali kupewa nafasi na Waziri wa utalii Hamisi kigangwala kutembelea vivutio vilivopo nchini hasa mlima Kilimanjaro nakujifunza vingi zaidi.
” Tumeanza kupanda mlima Kilimanjaro lakini vingine vingi vitafata lengo likiwa ni kuutangaza utalii wetu kwa nchi za nje ili kujua vitu tulivobarikiwa sisi Kama watanzania,”
Hata hivyo platnum ameeleza ujio huo wa Tamasha utakua ni mara ya Kwanza kwake kutumbuiza Dar es Salaam kwani hakuweza kufanya hivyo kutokana na kukosa kibali kwa mwaka Jana kutokana na utovu wa nidhamu uliofanyika .
“Niliweza kutumbuiza uwanja wa Taifa katika Tamasha la jamaa lililoandaliwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ,Basi pale niligusa gusa tu balaa lenyewe mashabiki na wapenzi wa lebo ya wasafi (WCB) wajitokeze novemba 9 mwaka huu katika viwanja vya posta jijini Dar es salaam,”
Pia amegusia swala la vijana kupima afya zao nidhahiri wamekua wakipata ushirikiano wakutosha kutoka Taasisi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi (TACAIDS) na kupewa fursa Kila mkoa kuungana nao na kutoa elimu juu ya kujikinga na kuepuka maambukizi ya ukimwi.
Hata hivyo amefafanua kuwa Wana lengo la kuwa tofauti katika Tamasha la mwaka huu hasa la Dar es salaam na mashabiki wategemee uwepo wa wasanii wengine wengi kutoka nje ya nchi lengo ni kupata burudani kabambe.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ouhBGC
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







