Jinala Penny limo katika orodha ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na
msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jina lake kamili ni
Penniel Mwingilwa. Huyu ni Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar.
Wiki hii yuko hapa kujibu maswali ambayo waandishi wetu Imelda Mtema
na Hamida Hassan walimuweka mtu kati.Ijumaa: Mambo Penny, naona sasa
hivi una gari nyingine, ile Toyota Brevis ambayo mpenzi wako wa zamani
Diamond alikununulia iko wapi?
Penny: (Kicheko)…kwa kweli namshukuru kwa kuninunulia ile gari ila
sasa hivi siko nayo, nimeamua kubadilisha, si unajua mtu lazima uende na
wakati?
Ijumaa: Mara ya mwisho kupanda daladala ilikuwa lini?
Penny: Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Nilipoanza tu kazi ya
utangazaji, nilipopanda daladala watu walikuwa wananishangaa sana
nikaona hiyo siyo poa, nikawa napanda teksi.
Ijumaa: Ulikuwa na Diamond mkaachana, hebu tuambie kwenye maisha yako
ungependa umpate mwanaume wa aina gani?Penny: Kwanza awe mchamungu,
pili anithamini lakini pia awe mtu muelewa. Yaani ajue ni wakati gani wa
kufanya maamuzi sahihi na awe tayari kunisikiliza.
Ijumaa: Nini ambacho kinakukwaza sana na hukipendi kabisa?
Penny:
Ni watu kuniongelea tena kwa mambo ambayo hawayajui kuhusu mimi.
Nakerwa sana na wanaofanya hivyo.Ijumaa: Ukiwa katika ‘stress’ au mtu
kakukwza na kukukosesha amani, kipi ambacho huwa unakifanya kurudisha
amani yako?
Penny:Nikiwa katika hali hiyo breki ya kwanza ni kanisani. Pale kwenye Kanisa
la St. Joseph pembeni kuna kakanisa kadogo.Kwa hiyo nakwenda pale,
nasoma Biblia na kusali kwa muda wa saa sita hivi kisha nikiondoka hapo
nakuwa sawa.
Ijumaa: Muda wa kuolewa ukifika na mwanaume akaja kwenu na ukatakiwa
utamke mwenyewe mahari yako, ungetaka mahari ya shilingi ngapi?Penny:
Sina makuu, nitamtaka mwanaume huyo ampe baba yangu juzuu na msahafu
halafu mama yangu apewe Biblia. Kama kutakuwa na pesa kidogo tutaipeleka
kwa watoto yatima.
Ijumaa: Mastaa wengi wa kike wanadaiwa kutojua kupika, wewe hili likoje kwako?
Penny: Kitu ambacho nitamshukuru mama yangu siku zote ni kunifundisha
kupika. Najua kupika vitu vingi sana tena vinakuwa vitamu mno, kasoro
ugali ndiyo unanishinda ila najitahidi kujifunza.
Ijumaa: Umeanza kujitegemea ukiwa na umri mdogo, vipi unajilindaje na vishawishi vya wanaume?
Penny: Wakati naanza kupanga tulikaa kama familia, tukajadili
ikaonekana naweza kukaa peke yangu japo bado nipo chini ya wazazi wangu.
Kuhusu vishawishi havinisumbui kwani najitambua.
Ijumaa: Kilichowasukuma mkaamua kupatana na Wema Sepetu ni kipi?
Penny: Sisi ni watu wazima, tuliona haileti picha nzuri kuwa maadui.
Sasa hivi tuko na amani na hatutaruhusu watu watugombanishe tena.
Ijumaa: Ni kwa nini unapenda kuvaa nguo fupi?
Penny: Vimini siwezi kuacha ndugu yangu kwa sababu nina mguu mzuri wa kuvaa hivyo, au wewe unanionaje?
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






