Shirika la Kutengeneza Ndege kutoka nchini Marekani la Boeing kwa kushirikiana na mashirika yasiyokua ya kiserikali ya The Foundation For Tommorow na Junior Achievement Afrika limewezesha kambi ya Ubunifu kwa Wanafunzi wa Sayansi Zaidi ya 100 kutoka katika Shule 7 za sekondari za jiji la Arusha kwa lengo la kuhamasisha masomo ya sanyansi na kuchochea ubunifu na ugunduzi wa teknolojia mbali mbali kwa vijana wa bara la Afrika.
Shule za sekondari zilizoshiriki katika kambi hiyo ya Ubunifu ni Pamoja na Arusha Science Secondary,Kilasara Secondari ,shepherd Secondary na nyinginezo.
Mratibu wa Mafunzo kutoka shirika la The Foundation For Tommorow Evelyn Kaijage amesema kuwa ushirikiano na shirika la ndege la Boeing kutoka Marekani unalenga kuwawezesha vijana kushiriki katika masomo ya sayansi na kufanya tafiti na buniifu ambazo zitasaidia kutatua changamoto zilizoko katika bara la Africa.
Evelyn ameongeza kuwa ufadhili wa Boeing na JA Africa utasaidia kupata idadi kubwa ya wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na kuwezesha kupata wataalamu waliobobea katika masuala ya sayansi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Juniour Achievement Africa (JA) Phil Mlambo amepongeza shirika la Boeing kwa kuwasaidia wanafunzi wa masomo ya sayansi kuwaza kibunifu Zaidi na kufikiria kutatua changamoto zinazoikabili jamii yao kupitia bunifu zao.
Kwa Upande wao wanafunzi walioshiriki kwenye kambi hiyo ya ubunifu akiwemo Elizabeth Cathbet kutoka Shule ya sekondari Arusha Science amesema kuwa kambi hiyo imewawezesha kupata uzoefu na maarifa kutoka kwa wabunifu mbali mbali na wanasayansi ili kuongeza ari ya wao kujikita Zaidi kwenye sayansi na ubinifu.
Asimwe Elly ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilasara kutokana na mwamko mkubwa wa masuala ya sayansi inaotokana na juhudi za TFFT tayari wameanza kubuni teknolojia mbali mbali ambazo zinahitaji ulinzi wa kisheria ili ziweze kuwanufaisha wabunifu.
SOMA HABARI NJEMA HAPA
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







