Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 11,2019, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Doto James amesema kwa kuzingatia mfumo huo imeiagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu kuwa taasisi zote za ununuzi nchini ziwe zimeungwa katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote.
Katibu Mkuu James amesema kuwa kuzingatia kwa fedha zitumikazo katika utekelezwaji wa miradi ya Serikali kwa kiasi kikubwa hutumika kupitia mifumo ya ununuzi wa umma na kwamba jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuliimarisha eneo hilo ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kupitia ununuzi wa bidhaa.
Amesema taasisi za umma ambazo tayari zimeunganishwa katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki ni jumla ya taasisi nunuzi 418 kati ya taasisi 540 sawa na asilimia 77.4 ya taasisi nunuzi zilizopo nchini zimeunganishwa na mfumo huo.
James amesema tangu kuanza kwa mfumo huo kumeongeza ushindani kwenye michakato ya ununuzi ,kuongeza ufanisi na hivyo kupunguza muda unaotumika katika michakato ya zabuni pamoja kuongeza uwazi hivyo kupunguza vitendo vya rushwa.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi Leonard Kapongo amesema baada ya kupewa maagizo na Serikali waliingia kazini kuongeza katika kutoa mafunzo kuhusiana na mfumo kwa maafisa Ununuzi na Tehama wa Taasisi za Umma.
Amesema hawataruhusu taasisi za umma kufanya nunuzi nje ya mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki kufikia Januari 31 mwaka ujao.
Mhandisi Kapongo amesema taasisi ambazo hazjaunganishwa wajiunge ikiwa ni pamoja na kugharamia mafunzo maakumu ya namna ya kutumia mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki.
Pichani kati ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar,kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS) ikiwa pamoja na Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri wa Fedha kuhusu matumizi ya mfumo huo.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga na kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo.
Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiwaonesha Waandishi wa Habari moja ya Nyaraka iliyokuwa na maelekezo ya uanzishwaji mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambapo amesema Serikali imeagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) ifikapo Disembe 31,2019 ihakikishe taasisi zote za ununuzi hapa nchini ziwe zimeungwa katika mfumo huo na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote. Picha na Michuzi JR.(MMG).
Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33EdhUD
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









