Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo balozi wa Denmark nchini Mheshimiwa Einar Hebogard Jensen amesema kuwa mkataba huo umeelekezwa katika sekta tatu ambazo ni programu za utawala bora, upatikanaji wa haki na haki za binadamu.
Katika makubaliano hayo Serikali ya Denmark imetoa msaada wa Krona milioni 7 sawa na takribani dola za kimarekani milioni 1, 049, 776 huku tafiti zikionesha kuwa kwa mwaka 2018 walitoa jumla ya dola za kimarekani milioni 63.
Balozi Jensen amesema kuwa Denmark inaamini kuwa ili kufikia maendeleo lazima misingi ya uwazi, uwajibikaji na usawa wa kijinsia iwepo na wamekuwa na ushirikiano duniani kote na kupitia UNDP nchini Tanzania wamekuwa wakishiriki na kufanya kazi kwa pamoja katika kuboresha shughuli za bunge, utawala bora pamoja na taasisi na vituo mbalimbali za haki za binadamu.
Aidha amesema kuwa watanzania wanazijua haki zao kwa kufuata sheria na hiyo ni kutokana na ukomavu wa demokrasia nchini.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Natalie Boulcy amesema kuwa Denmark ni moja kati ya nchi 10 zinazoshirikiana na kutoa msaada mkubwa kwaUNDP hasa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora na ulinzi.
Natalie amesema kuwa msaada utawafikia watu wengi zaidi hasa vijijini pamoja na kusaidia sekta mbalimbali zikiwemo tume ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) hasa katika kuwajengea uwezo, ikiwa ni pamoja na kuwezesha uchapishaji wa ripoti za haki za binadamu kwa kila mwaka na kuzimbaza kote nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na katiba na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali .
Pia msaada huo utaelekezwa katika makundi mbalimbali wakiwemo wanawake na watoto, ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa serikali (DPP) kupitia Wizara ya sheria pamoja na vituo vya haki za binadamu na utawala bora.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2JtFgPq
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33











