
Katika muongo uliopita sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania imeshuhudia ukuaji mkubwa na kuongezeka kwa kasi kwa maendeleo ya teknolojia. Katika wakati huu makampuni ya simu yamefanya kazi kubwa kuwapa wateja huduma bora na ubunifu ambao umeleta mabadiliko makubwa ya kidijitali.
Sambamba na hilo, sekta hii pia imekuwa moja ya sekta bunifu zaidi katika bara la Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara hasa katika teknolojia bunifu kwenye kufanya malipo kwa njia ya simu, huduma za bima na afya. Ni muhimu kwamba maendeleo haya yote kwenye sekta hii yawe na tija ya muda mrefu kwenye maisha ya Watanzania. Mfano kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi kumeongeza idadi ya ajira hasa kwa wenye simu janja sio tu kwa watu binafsi lakini hata kwenye biashara na taasisi za kiserikali.
Huku sekta hii ikiendelea kutanuka zaidi, yako mengi ya kufanya ili kuhakikisha inaendelea kuwa juu na kutupa faida zaidi na hakika hatua zimeanza kuchukuliwa za aina mbalimbali ili kuhakikisha hilo. Mfano, Novemba mwaka jana ilitangazwa kuwa Tigo na Zantel wameunganisha huduma zao ili kuongeza nguvu na kuboresha huduma kwa wateja wa kampuni zote mbili. Hatua kama hizo ni muhimu sana. Wataalamu wa sekta ya mawasiliano wanaweka bayana kuwa kampuni chache zenye ubora sokoni ni bora kwa wateja na taifa kwa ujumla tofauti na kuwa na utiriri wa kampuni lakini zenye huduma zisizo bora. Kampuni zikifanya kazi pamoja kama mfano wa Tigo na Zantel huwekeza vizuri zaidi faida ili kutoa huduma bora na za kibunifu zaidi.
Mwaka 2020 umeanza na tunaelekea kuanza muongo mwingine mpya, tutarajie matunda haya ya siku za karibuni ambayo tumeyaona kwenye sekta ya mawasiliano ya simu kuwa ni mwanzo tu, kwani sekta hii ina mengi makubwa sana ya kutupatia Watanzania.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sZtkiB
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






