RC Dodoma atoa wito huu kwa Wizara ya Katiba na Sheria
Imewekwa na Masama Blog

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa Wizara ya Katiba na Sheria kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kujitojeza kwa wingi kupata Elimu na Msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayotekelezwa na wizara hiyo.
RC Dodoma ametoa wito huo Agosti 5, 2025 Jijini Dodoma wakati alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane Nzuguni.

Senyamule amesema kuwa wananchi wanatakiwa kunufaika na Msaada wa kisheria wakati huu wa maonesho kwa kuwa wamekuwa wakiwafuata watu ambao hawana uelewa na masuala ya Kisheria.
“Kama mko hapa mjitangaze ili wananchi waje kwa wingi, wapate huduma za Msaada wa Kisheria kwa kuwa mara nyingi wamekuwa wakitufuata lakini tunashindwa kuwasaidia kwa kuwa wengi wetu hatuna utaalam na masuala ya kisheria” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Msaada wa Kisheria, Osborn Paiss amefafanua kuwa Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki maonesho ya Nanenane kwa kuendelea kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia pamoja na kutoa elimu kuhusiana na Utajiri asilia na maliasili za nchi pamoja na elimu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora bure.

“Tuko katika viwanja hivi vya Nanenane Nzuguni katika Maonesho ya Wakulima, tunaendelea kutoa huduma za Msaada wa Kisheria, Elimu kuhusiana na Utajiri Asilia na Maliasili za nchi, Haki za Binadam, Uraia na Utawala Bora, tunawakaribisha wanachi wote kuja kupata huduma maana zinatolewa bure kabisa” amesema Osborn.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






