Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewasilisha tamko linalohusu Mapato,Rasilimali na Madeni ya viongozi katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria na kikatiba.
Tamko hilo limewasilishwa katika ofisi hizo kanda maalumu ya Dar es salaam na katibu wa Rais, Bwana Ngusa Samike ambaye ametumwa na Mhe Rais akiwa mapumzikoni Chato na limepokelewa na Kamishna wa Sektretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Jaji mstaafu Harold Nsekela.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Jaji mstaafu Nsekela amesema kitendo alichokifanya Mhe.Rais kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (D) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, Rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria no 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.
Jaji mstaafu Nsekela akatumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wengine kutumia siku 2 zilizobaki kufanya hivyo kabla ya tarehe 31 Desemba katika kutekeleza takwa hilo la kisheria na kikatiba






from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37km5jO
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






