MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amewataka watumishi wa Chuo hicho kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za utumishi wa umma.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imesema hayo yamesemwa na Prof. Mwakalila wakati akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya uongozi wa Chuo hicho na wafanyakazi lengo likiwa ni kukumbushana, kuelekezana na kujipanga kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo mwaka 2019/20.
“Sisi ni watumishi wa umma na utumishi wa umma ni dhamana hivyo tusikubali kuchezea fursa hii tuliyonayo ni vyema tukatimiza Wajibu wetu kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za Utumishi wa Umma,”anasisitiza Prof. Mwakalila.
Pia Mkuu huyo wa Chuo amewataka wafanyakazi wote kuwa na uelewa wa dira ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwa ni kitovu cha utoaji wa maarifa bora kuhusu ubunifu, uvumbuzi na kuendeleza Amani na Umoja.
Amesema Chuo hicho pia kina jukumu la kutoa mafunzo ya uongozi na maadili,mafunzo ya Kujiendeleza na Kufanya tafiti zinazotatua changamoto katika jamii.
Profesa Mwakalila pia ameelezea baadhi ya mafanikio ya Chuo hicho kuwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, ambapo tayari vyumba vyote vya madarasa vimefungwa viti visivyohamishika, Madarasa yamefungwa vifaa vya kisasa vya kufundishia, idadi ya vitabu imeongezwa kwenye Maktaba kwa kampasi zote mbili, ikiwemo ya Kivukoni na ile ya Karume- Zanzibar.
Pia amebainisha baadhi ya mikakati ya Chuo hicho kuwa ni ni pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, ujenzi wa hosteli kwa kampasi ya Karume- Zanzibar na kuongeza bajeti kwa ajili ya tafiti mbalimbali lengo likiwa ni kutatua changamoto katika jamii.
Prof. Mwakalila amewataka viongozi wenzake wakiwemo Manibu wa Chuo hicho, Wakuu wa idara na Vitengo katika Chuo hicho kuhakikisha wanatenda haki kwa watumishi walio chini yao ikiwa ni pamoja na kujiepushe na vitendo vyote vya ukabila, dini au Rangi.
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
30/10/2019
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila akizungumza leo wakati anazungumzia na uongozi wa Chuo hicho
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mkutano huo
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36maXmQ
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








