Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ( ATCL), Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni, inashikiliwa nchini Canada na kesi ipo mahakamani.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Mabalozi mbalimbali, Waziri Kabudi amesema kuwa, ndege hiyo inashikiliwa baada ya kufunguliwa kwa kesi mpya, kesi ambayo imefunguliwa na Mkulima aliyeshindwa Kesi aliyoifungua nchini Afrika Kusini.
Profesa Kabudi ameongeza kuwa, Serikali imekasirishwa na vitendo vya ndege zake kushikiliwa nchini Canada, na kwamba tayari amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada hapa nchini kumueleza kuhusu jambo hilo.
Waziri Kabudi pia ametumia hafla hiyo kuwataka Mabalozi hao wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mataifa mbalimbali, kwenda kusimamia vizuri matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali, kwa kuwa kumekua na matumizi mabaya ya fedha kwenye Ofisi za Ubalozi.
Ametolea mfano Ubalozi wa Tanzania huko Addis Ababa – Ethiopia ambapo kumekua na ubadhirifu mkubwa na fedha na kuongeza kuwa kwa sasa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inaendelea na uchunguzi.
Katika hafla hiyo, Rais John Magufuli amewaapisha Mabalozi Watano ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2XH0lLG
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







