Naibu KM(OR-TAMISEMI) Mha.Mativila aongoza Manaibu Makatibu wakuu Kutembelea Nane Nane,Waipongeza TARURA

#Waipongeza kwa kuwafungulia barabara wakulima
Dodoma
Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakiongozwa na Mhandisi Rogatus Mativila Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Sospeter Mtwale – Naibu Katibu Mkuu (Utawala na Rasilimali Watu) na Prof. Tumaini Nagu – Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea Banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

Makatibu Wakuu hao wamepatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa Wakala huo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Bi. Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango ya TARURA inayohusu uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Naibu Katibu Mkuu Sospeter Mtwale amewapongeza TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kufungua barabara hususan maeneo ya wakulima,wavuvi na wafugaji na hivyo kuwarahisishia kusafirisha mazao yao.
Pia amesema barabara hizo zimesaidia waendesha bodaboda na waendesha vyombo vya moto vingine na hivyo kupata ajira hivyo kuwataka kuendelea kuboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika wakati wote.




Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






