Issa Mnally na Richard BukosKIJANA
mmoja mtanashati, aliyefahamika kwa jina la Faraja Adam mkazi wa
Makongo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinusurika kipigo kutoka
kwa wakazi wa Mabibo Jeshini baada ya kukutwa sebuleni kwa mpangaji wa
nyumba moja aliyefahamika kwa jina la Rhobi Chacha.
Majirani wa mpangaji huyo waliliambia gazeti hili kwamba walimuona
kijana huyo akiambaaambaaa na ukuta wa nyumba hiyo kisha kuingia ndani
kwa kunyata, kitu kilichowapa shaka na kuamua kumpigia simu jirani yao
kumweleza juu ya ujio wa kijana huyo.
Majibu waliyopewa na mpangaji huyo yaliwafanya majirani hao
kujikusanya, wakiwemo walinzi wa kimasai wanaolinda maeneo hayo na
alipofika Rhobi, ndipo walipoingia ndani na kupigwa na butwaa kumkuta
‘sharo’ huyo akiwa amejilaza kwenye kochi sebuleni, akiwa ameshikilia
rimoti akiibonyezabonyeza kama yupo nyumbani kwao.
Alipoulizwa
kilichompeleka hapo, alikosa cha kujibu, akionekana kuchanganyikiwa.
Baada ya kutishiwa kipigo cha kumwitia mwizi kwa kuingia kwa watu bila
wenyewe kuwepo, aliomba aachwe kwa maelezo kuwa alimfuata dada wa kazi
wa nyumba hiyo.
“Jamani mimi nina ndugu zangu wakubwa sana serikalini, naomba
msinifanye chochote kile, nimekuja kwa Jesca (house girl) kwani ni
dadangu kabisa,” alijitetea kijana huyo.
Jesca baada ya kuulizwa uhusiano wake na kijana huyo alikosa cha
kusema, lakini simu yake ya mkononi ilipopekuliwa, ilikutwa ikiwa na
meseji alizokuwa akitumiana na kijana huyo, zilizoashiria mapenzi.
Baadaye wawili hao walidhibitiwa na kupelekwa kituo cha Polisi cha
Urafiki ambako mzazi wa Faraja alipoitwa, alitaka mwanaye huyo alazwe
rumande ili iwe fundisho kwake aachane na tabia hiyo.
Naye Rhobi, aliliambia gazeti hili kuwa tabia ya msichana wake huyo
wa kazi imebadilika katika siku za hivi karibuni na kwamba mara kadhaa,
amekuwa akikuta kitanda chake kikiwa kimevurugika tofauti na
alivyokiacha
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





