Kwa mara ya kwanza tangu walipomwagana, mastaa wawili Bongo,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wanadaiwa
kuoneana aibu walipokutana laivu.
Akiwa na mtangazaji mwenzake, Edzen Jumanne, wikiendi iliyopita
Jokate alidaiwa kushindwa kumbana Diamond kwa maswali wakati akimhoji
kwenye kipindi kitakachoruka hewani hivi karibuni kupitia TV1.
Baadaye Diamond alitupia mtandaoni picha akiwa na zilipendwa wake
huyo hivyo kuibua mjadala mzito kuwa huenda bado wanapendana huku
wenyewe wakipiga kimya.