Na Charles James, Michuzi TV
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mussa Mwakitinya amewataka vijana wa Chama hicho kusimama mstari wa mbele kumtetea Rais Dk John Magufuli kwenye mitandao ya kijamii.
Mwakitinya ameyasema hayo wakati akizindua mashina ya wakereketwa wa Umoja wa Vijana 13 katika matawi saba ya Kata ya Mbagala Kuu Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
” Rais Magufuli anafanya mambo ambayo sisi wote hatukuwahi kutegemea yatafanywa Tanzania, Elimu bure, Nidhamu kwa watumishi, ujenzi wa reli ya kisasa na bwawa la kufua umeme, mtandao wa barabara za lami Nchi nzima, na zaidi ujenzi wa Tanzania ya uchumi wa viwanda, tusimame kumtetea Rais wetu dhidi ya watu wasioitakia mema Nchi yetu, ” amesema Mwakitinya.
Katika ziara hiyo Mwakitinya aliambatana na Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa, Gertrude Ndibalema ambaye alijiunga na CCM ambapo nae alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri mambo makubwa yanayofanywa na Rais Magufuli.
” Sisi ndio msingi wa Maendeleo katika Taifa letu, Serikali ya CCM chini ya Dk Magufuli imeonyesha dira kwa Taifa letu ni jukumu letu kumsemea vizuri Mwenyekiti ambaye pia ndio Rais wetu, tusiogope twendeni mbele na kueleza yale yote mazuri yanayofanywa na Serikali yetu,” amesema Ndibalema.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MBthkx
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








