Na Ahmed Mahmoud,Killimanjaro.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annaclair Shija amewasimamisha watumishi wawili wa hospitali ya wilaya hiyo akiwemo Afisa Tabibu kwa kudai na kupokea rushwa ya shs. 15,000/= kutoka kwa mama mwenye mtoto mchanga mgonjwa wakike mwenye umri wa miezi mitano wa kijiji cha Vunta kilichopo ukanda wa milimani mwa wilaya hiyo.
Shija amechukua hatua hiyo baada ya afisa tabibu huyo Kimweri kihiyo amesimamishwa kwa kumwandikia upasuaji mtoto huyo ambao hakustahili na kudai rushwa hiyo huku mlinzi daniel kihara alimuuzia dawa kutoka bohari ya serikali kwashs. 4,500/ kwa mama wa mtoto huyo ambaye alistahili apewe mtoto wa miaka 12.
Aidha amesema, vitendo vya aina hiyo vimekuwa vikiidhalilisha serikaliambayo imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia 90 na kitendo cha kumwandikia dawa na upasuaji ambao hakustahili ni sawa mauaji .
Muuguzi wa hospitali hiyo bw Fabian Bulili amesema kuwa afisa tabibu huyo ambaye hakuwa kazini anaonyesha alikuwa na tabia ya kuwaandikia dawa wagonjwa kwa ushirikiano na watumishi wasio waaminifu na kujipatia fedha kuikosesha mapato halmashauri
Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo eliabu mgonja wameipongeza hatua hiyo na kueleza kuwa watumishi wa aina hiyo wanastahili kufukuzwa kazi ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afya bila kudaiwa rushwa.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36zQHgO
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







