Baadhi ya Wananchi wakiwa wamesimama pemezoni mwa barabara kumlaki mgombea mwenza wa urais CCM alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma kufanya mikutano yake ya kampeni.
Mgombea mwenza akizungumza na wananchi waliomsimamisha njiani kuwasilisha kero zao.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa
CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kijiji cha Mlyabibi, Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea
mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi
ilani ya CCM.
Wananchi na wanaCCM wakimshangilia mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili mkoani Kigoma kuanza ziara yake ya kampeni. Mama Suluhu kawasili mkoani Kigoma na kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigoma Kusini, Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Baadhi ya vijana waliohama kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na CCM wakiwa wamemnyanyua juu mmoja wa viongozi aliyewashawishi kujiunga na chama hicho mara baada ya kupokelewa na mgombea mwenza wa CCM kwenye mkutano wa kampeni mjini Uvinza Kigoma. Zaidi ya vijana 60 wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Kata ya Uvinza, Himid Kisobwe wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mama Samia Suluhu.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33














