Mha.Lightness Salema Achukua Fomu ya ubunge jimbo la Mwanga,asema Mwanga sasa ni zamu ya Wanawake

Masama BlogMAGAZETISIASAKITAIFAMATUKIO5 months ago249 Views

Mhandisi Lightness Ladislaus Salema amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro huku akisema Mwanga ni zamu ya kinamama kupata nafasi ya uwakilishi kwani ni muda mrefu jimbo hilo linaingozwa na kufanyiwa kazi kubwa ya uwakilishi na wakina baba na saaa ni wakati wa wao kupata ahueni kusaidiwa na wanawake na yeye yupo tayari kuwawakilisha kinababa na kinamama wakazi wa Mwanga bungeni.

Aidha Mhandisi Lightness Salema ni mtanzania mzalendo na mpenda maendeleo ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Rughwini, Lembeni – Mwanga Kilimanjaro.

Kwa sasa Mhandisi Lightness Ni mfanyabiashara, mshauri wa maendeleo na mjasiriamali aliyebobea katika sekta ya madini, kilimo, utalii, uwekezaji, na ujenzi.

Pia ni Kiongozi wa asasi ya Wanawake wa Jumuiya za Madola – Afrika (Commonwealth Business Women Africa).

Mhandisi Lightness amechukua fomu leo tarehe 29, Juni 2025 kutia nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mwanga kupitia chama cha mapinduzi CCM na ameslonyesha wazi yuko tayari na anaweza!

Masama Blog inamtakia kila la Heri Mhandisi Lightness L.Salema katika hatua hii muhimu ya kuelekea uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi jimbo la Mwanga

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...