Mbao Yajipanga Kuivurugia Tena Yanga

7 years ago72 Views

Mbao Yajipanga Kuivurugia Tena Yanga

MBAO FC ya Mwanza, imesema balaa la kufungwa ambalo Yanga imekumbana nalo juzi Jumamosi kutoka kwa Simba, ndilo itakalokutana nalo Jumatano kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Yanga itapambana na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku ikiwa imetoka kuchezea kichapo cha bao 1-0  kutoka kwa Simba.

Msemaji wa Mbao FC, Crisant Malinzi, ameliambia Championi Jumatatu kuwa: “Tunaendelea na maandalizi yetu kwa ajili ya mechi hiyo, na lengo letu ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi.

“Kwa hiyo Yanga waje waki jua kabisa kuwa hakuna watakachoambulia katika mechi hii kwani mbinu zao na mipango yao yote kocha wetu, Allu Bushiri anayo na anajua jinsi ya kuwazuia,” alisema Malinzi. Mbao FC wapo nafasi ya saba wakiwa na pointi 33 wakati Yanga wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 58

from UDAKU SPECIAL BLOG https://www.udakuspecially.com/2019/02/mbao-yajipanga-kuivurugia-tena-yanga.html
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.