MAHUSIANO:HAYA NDIYO MAMBO YANAYOCHANGIA KUPOTEZA HISIA ZA MAPENZI.
UKWELI ni kuwa watu wengi wanaodai hawatosheki katika mapenzi,ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi.Watu hao hawaangalii uwezo,nafasi,hisia na afya ya kukutana kimwili.Jambo muhimu analopaswa kuzingatia
kila aliye kwenye uhusiano ni kwamba,kama unataka kutosheka na penzi la
mpenzi wako,ni lazima utosheleze kwanza akili yako.Unapaswa kuamini
kuwa uliyenaye ni bora na kwamba kama ziko kasoro,lililo la msingi ni
kuzizungumza na kuziondoa.Ukweli
ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki mbali ya yale niliyotaja
hapo juu,lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao
wa zanani,ambao labda walikuwa na uwezo mkubwa zaidi katika tendo kuliko
akiye naye sasa.Hata hivyo,wakati
mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri,kama
wangekuwa nao hadi sasa huenda nao wasingeweza kuendelea kuwaimara.Hii ni kwa sababu,watu wengi báada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.Zipo sababu
nyingi za hali hiyo,mojawapo ni kutobadilika kwa mazingira au wapenzi
kuanza kutoelewana kwa sababu mbalimbali kama vile kutojaliana na kadhalika.NGUVU ZA KIJINSIA.Kama
hukuwa unafahanu,Ni kwamba idadi ya wanaume wasio na uwezo wa kufanya
vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka.Tafiti zinabainisha kuwa wastani
wa ndoa nne kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliwa
na tatizo hilo.Pia wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume,kwanba kama siyo kuwa na uwezo mdogo,basi hukosa kabisa nguvu za kuendelea.Wengine wanaweza kuanza,lakini hawawezi kuendelea na wengine hata kuanza nishida.Idadi kubwa
ya wanaume bado wanasumbuliwa na tatizo hili hasa kwa sababu ya
kutokuwa tayari kuchukua hatua hasa za kuzingatia ushauri.Ziko sababu nyingi za kukumbwa na hali hii,ikiwemo ulevi,kutofanya mazoezi,kujichua au utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta.Hata hivyo kwa kuzingatia tiba sahihi ya vyakula,mtu anawezakupona.Kwa mfano
kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa kwa ustadi kama
pilipili,parachichi na kadhalika vinaweza kunfanya mtu kuondokana na
tatizo hilo.Wengi
wa watu walio kwenye ndoa za miaka mingi,wanafanya mapenzi kwa sababu
tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja,lakini siyo kwa sababu ya kuwa na
hisia kali.Matokeo yake ni wanandoa wengi kupata msisimko mdogo karika
tendo la ndoa wanapokuwa na wenza wao.Hata hivyo,kwa kuzingatia utaalamu,wanaweza kuwa na furaha katika ndoa yao
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News