Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu ,Uwekezaji ,Angela Kairuki akizungumza wakati wa mchezo wa fainali ya Mashindano ya Angela Kairuki Cup 2019 alipoalikwa kama mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhi zawadi kwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Katibu wa Cha soka wilaya ya Same,Nathaniel Msuya akisoma taarifa fupi ya mashindano ya Angela Kairuki Cup wakati wa kuhitimisha ligi hiyi iliyodumu kwa muda wa miezi miwili ikishirikisha jumla ya timu 54 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Same.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji Angela Kairuki akisalimiana na waamuzi wa mchezo huo.
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Ujamaa fc Kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kisiwani United kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali baina ya timu hizo mbili.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kisiwani united kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Ujamaa fc kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kwa timu hizo ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Isaya Mungulu.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mchezo wa fainali baina ya timu za Kisiwani united na Ujamaa fc zikimenyana kuwania ubingwa wa mashindano ya Angela KAiruki Cup 2019 .
Mashabiki wa timu ya Kisiwani United wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa na kutangazwa mabingwa wapya baada ya kuchapa timu ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi Hedaru.Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akikabidhi Kombe kwa nahodha wa timu ya Kisiwani united mara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya soka ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1.
Waziri Kairuki akikabidhi fedha taslimu ,kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa nahodha wa timu ya Kisiwani United mara baada ya kuibuka Mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Waziri Kairuki aikabidhi pipikipi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Kisiwani United baada ya kuibuka mapbingwa wapya wa mashindano hayo. Katika mchezo huo mabao ya washindi yalipachikwa na Wachezaji Ally Rajab kunako dakika 35 ya kipindi cha kwanza huku mchezaji Juma Makumbi akipigilia msumari wa pili uliowapatia ubingwa timu ya kisiwani fc.
Bao kwa upande wa timu ya soka ya Ujamaa fc iliyokuwa imesheheni wakongwe limefungwa na mchezaji Ezekiel Ombeni kunako dakika ya 40.
Katika mchezo huo ilishuhudiwa mchezaji Ally Mbaga akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa pembeni wakati akilalamikia maamuzi yake dhidi ya bao lililofungwa n timu ya Ujamaa fc.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ok0hyz
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33












