Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
SUALA la baadhi ya mitandao ya simu nchini kufunga laini kabla ya tarehe elekezi ya kufunga laini hizo ambayo ni Desemba 31 mwaka huu.
Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa kufikia Desemba 31 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole na namba za kitambulisho cha uraia zinazotolewa na (NIDA) zitakatwa na kile kinachoelezwa kuwa baadhi ya mitandao imeanza kufunga laini hizo ni kukumbushwa kuwa watazikata laini zote zisizo na usajili.
Akijibu hoja ya kwanini baadhi ya makampuni ya simu yamefunga laini za simu kabla ya wakati Mhandisi Kamwelwe amesema;
“Zoezi la usajili litakamilika tarehe 31 Desemba mwaka huu, na tutakata laini zote zisizosajiliwa kwa kutumia namba za NIDA na alama za vidole” amesema.
Aidha amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakiibiwa kutokana na umiliki holela wa laini za simu ambapo mtu mmoja anaweza kumiliki laini za simu zaidi ya mia moja.
“Kenge hasikii hadi damu itoke puani, mlikuwa mnashtuliwa tutakata laini zote zisizo na usajili kufikia Desemba 31 mwaka huu” amesema.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiwaji saini wa makubaliano ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya umoja wa shirika la Posta Barani Afrika, Pan African Postal Union (PAPU) umoja ulio na nchi wanachama 45 na jengo hilo litajengwa jijini Arusha Tanzania.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QbngeB
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







