Baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana, Jumanne wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya African Lyon na Simba, Kocha wa African Lyon, Suleyman Jabir amesema kuwa Simba ilibebwa kupata matokeo.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, imeshuhudiwa Simba ikiitandika African Lyon kwa mabao 3-0, ambapo baada ya kocha Jabir kulalamikia maamuzi ya uwanjani, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara akaibuka na kujibu tuhuma hizo.
Manara amesema, “hayo maneno ya kubebwa ni ya kawaida, hata Yanga walisema, kila timu inasema, basi tufanye kila timu iwe inakuja na makocha wake na madaktari wake ndio wawe waamuzi kwasababu hizi lugha za kihuni”.
“Tatizo la watu wanaaminishana mambo ya kubebwa bebwa, Simba ina uwezo wa kimpira kuliko klabu yoyote Tanzania kwahiyo yoyote atakayekuja ataona anaonewa tu. Kwa ‘level’ ya Tanzania sisi ni Alpha na Omega”, ameongeza Manara.
Baada ya mchezo huo sasa Simba inarejea Jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya ‘Wana lambalamba’ Azam FC utakaopigwa Ijumaa, Februari 22.
from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2T790ab
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







