Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera hadi Novemba 20, mwaka huu kufuatia upande wa Mashtaka kudai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh milioni 173.
Wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo kuwa Kesi hiyo leo Novemba 7, ilipangwa kwa ajili kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika pia Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ameteuliwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu hivyo ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo wakati ikisubiri ipangiwe Hakimu mwingine wa kuendelea kuisikiliza.
Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Katika shtaka la kwanza, Kabendera anadaiwa kujihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Pia anadaiwa kuwa bila ya sababu, alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34CzBy0
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







