Na Ripota Wetu,Michuzi TV
KIJANA Mtanzania Erick Venant amepokea tuzo ya Legacy jijini London,ikiwa ni ya kutambua mchango wake katika kupambana na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa(Antimicrobial resistance) na hasa kuongeza uelewa kwenye jamii na kutia hamasa ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tatizo hilo.
Erick amepokea tuzo hiyo Novemba 26 mwaka 2019, ambapo juhudi zake zinapaswa kuwa muhimu katika kuboresha afya ya ulimwengu. Akiwa Uingereza Erick amepata nafasi ya kukutana na Prince William katika makazi ya Kifalme, Kengstone palace ambapo walijadili kwa ufupi kuhusu tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
Kwa mujibu ya magazeti ya nchini Uingereza yameripoti jinsi Prince William alivyotumia lugha ya Kiswahili mara kadhaa wakati wa mazungumzo hayo.Erick ni miongoni mwa vijana 20 duniani waliochaguliwa kupokea tuzo ya Legacy waandaji wa tuzo hiyo “The Diana award” na kwamba inaelwzwa kwamba vijana wote waliochaguliwa wana mchango mkubwa kwenye jamii.
Washindi wengine wametoka mataifa ya Uingereza, Malaysia, India,Canada, Nigeria na Nepal.Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Elizabeth Nyamayaro na mtendaji mkuu wa Shirika la ndege la Uingereza Alex Cruz ni miongoni mwa waliounda jopo la majaji 14 waliokutana kuchagua washindi 20 wa tuzo hii kutoka miongoni mwa washindi wa tuzo ya Diana award wa mwaka 2018 na 2019.
Sherehe za Utoaji wa tuzo zilifanyika katika ukumbi wa Old Royal Naval College,Greenwich-London na kuhudhuriwa na kaka mkubwa wa Princess Diana, Earl Spencer.Tuzo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.Tuzo za Diana award na Legacy award hutolewa kama kumbukumbu ya Princess Diana wa Wales aliyefariki mwaka 1997.Watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo hilo.
Kijana Erick Venant akiwa na tuzo yake ya Legacy jijini London,chini Uingereza.
Kijana Mtanzania Erick Venant, akipongezwa na Prince William baada ya kukaribishwa kwenye makazi ya kifalme,Kingstone Palace kwa kupokea tuzo ya Legacy jijini London,chini Uingereza.Tuzo hiyo imetolewa Novemba 26,2019.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34HLzXm
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33










