ALIYEKUWA Katibu Kata wa Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari amekihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Chahasi amerudisha kadi ya CUF na kukabidhiwa ya CCM leo na Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed katika mafunzo ya viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya kata.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Chahasi amesema amefanya uamuzi wa kuhamia CCM kutokana na haki walizokuwa wakizipigania akiwa CUF kuanza kutekelezwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mshikamano uliopo ndani ya chama hicho tawala.
Amesema Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amekuwa akipigania haki za kiuchumi hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo sasa wametambulika na serikali.
“Kwa sasa machinga tumeanza kupata neema ya kutekeleza shughuli zetu bila kubughudhiwa na sasa tumepatiwa vitambulisho vya kutambua shughuli zetu,” amesema Chahasi. Ameongeza kuwa Mungu amemteua Rais Magufuli kuwakomboa wanyonge hivyo Watanzania hawana budi kumuunga mkono.
Aidha aliwataka kundi alilokuwa anafanya nalo kazi maarufu kama Mungiki kumuunga mkono uamuzi wake kwa kuwa siasa zinabadilika na kila mmoja anahitaji maisha bora, uchumi na maendeleo kwa Taifa.
Kwa upande wake Cholaje amesema wanaamini Chahasi atakuwa na msaada mkubwa katika CCM kwa kuwa ataonesha mapungufu waliyonayo vyama vya upinzani kwa kusaidia kuyaeleza kwa wananchi.
“Ni siku ya neema kwa ngazi zote za chama kuanzia tawi hadi taifa kwa kuwa tumemchukua mpiganaji wa CUF ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa Lipumba,” amesema Cholaje.
Aliongeza kuwa wanatarajia Chahasi atakuwa sehemu ya Kampeni kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Chahasi amekuwa mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999 na anatajwa kuwa alikuwa ni sehemu ya wanamkakati wa waliofanikisha ushindi wa udiwani wa sasa kupitia CUF katika Kata ya Makurumla, Omari Kombo ‘Kijiko’.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akipa kiapo cha uaminifu kwa chama pamoja na viongozi wa CCM.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akisindikizwa kuingia ukumbini na mmoja wa viongozi wa CCM.

Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed, akizungumza na wana CCM baada ya kukabidhi kadi kwa aliyekuwa Katibu wa CUF Makurumla, Shomari Chahasi.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2JhIB4k
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






