Balozi wa Mtwara na Mwandishi wa vitabu nchini Bw. Joel Nanauka amekutana na kufanya Mazungumzo na katibu mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.
Katika mazungumzo hayo wamejadiliana mambo mbalimbali ikiwemo mchango wa Ndg Nanauka katika program mbalimbali za uimarishaji wa chama kwa ujumla na program maalumu zinazohusu vijana.Ndg Joel Nanauka , alimpongeza Katibu Mkuu kwa kazi kubwa anayofanya na alimhakikishia kuwa yuko tayari kuendelea kutoa mchango wake kwa chama kuanzia ngazi ya Taifa hadi chini kabisa Kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote.
Moja kati y avitabu vilivyoandikwa na mwandishi huyu mahiri ambaye ni Balozi wa Mtwara Bwa.Joel Nanauka na vitabu vyake vimeshawanufaisha watanzania wengi.Ndg Nanauka ambaye ni balozi wa Mtwara, alitumia nafasi hiyo pia kuwasilisha mambo mbalimbali ya kisekta yenye manufaa kwa mkoa wa Mtwara.Baada ya Mazungumzo, Ndg Nanauka alimkabidhi Katibu Mkuu Zawadi ya baadhi ya Vitabu alivyoandika na kumtakia kila la Kheri katika mkutano Mkuu maalumu wa CCM Taifa unaofanyika tarehe 01.04.2022.
Kabla ya kutoka katika ofisi za makao makuu ya Chama hicho Jijini Dodoma Nanauka alisema
“Binafsi nimefurahi na kufarijika sana kuonana na katibu mkuu wa Chama Chetu cha Mapinduzi Ndugu Chongolo,kwani nimetamani wasaa huu muda mrefu na nimejifunza mengi kutoka kwake pia tumekuwa na mazungumzo yenye manufaa sana kwetu,na nimemuahidi kutangaza mema yanayofanywa na chama cha mapinduzi kwa wana Mtwara na Watanzania kwa ujumla,Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Kazi Iendelee.
Alimalizia Ndugu Nanauka.
Picha juu ikimuonyesha Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Cde Daniel Chongolo leo baada ya kukutana na Ndg Joel Nanauka na kufanya naye mazungumzo katika ofisi Kuu za CCM jijini Dodoma ambapo Ndugu Nanauka alimpa vitabu ambavyo yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa vitabu hivyo kama ishara ya kutambua mchango wa katibu mkuu huyo kwa Chama Cha Mapinduzi..
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33










