Joel NANAUKA Akabidhiwa tuzo Muhimu na Mhe Rais Mwinyi,Amshukuru Rais Samia

1 year ago102 Views

 Muelimishaji jamii maarufu nchini Bw. Joel Nanauka akikabidhiwa na Mhe Rais Hussein Ali Mwinyi tuzo maalumu ya“LifeTime Mentorship Excellence Award”

Katika kuadhimisha wiki ya Vijana Duniani, kongamano kubwa limefanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort lililoandaliwa na Global Youth Empowerment Institute Bw.Joel Nanauka ameshinda tuzo katika kipengele cha “LifeTime Mentorship Excellence Award” .

Katika tukio hilo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Hussein Ali Mwinyi alitoa tuzo maalumu ya  kutambua mchango katika kukuza vijana.

Joel Nanauka amekabidhiwa tuzo ya “LifeTime Mentorship Excellence Award” inayotambua mchango wake katika kukuza rasilimali watu, hasa vijana nchini Tanzania.

Mhe Rais Mwinyi amewahimiza vijana kuendelea kuchangia mabadiliko chanya kwenye Jamii huku akiwahikikishia kuwa Serikali itaendelea kuwatengenezea mazingira mazuri na kuwasapoti katika shughuli zao.

Akiongea Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mhe Rais Mwinyi Bw.Nananuka amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu ,Familia yake bila kuwasahau wale wote wanaomuombea na kumuunga mkono kwa njia moja au nyingine hasa kwa kuendelea kusoma maandiko yake kama vitabu nk. akiwepo Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaamini amekuwa mmoja wa watanzania na viongozi anaowaona wakiendelea kuwatia moyo watu wanaoelimisha jamii kwa kuwa kiongozi anayependa jamii yenye kujitambua hasa kupitia elimu na maandiko mbalimbali jambo analoamini ndilo moja ya njia bora ya kujenga jamii imara  na yenye kufikia malengo kupitia welimishaji kama yeye bila kuwasahau viongozi wa dini 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.