Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Shirika la Saidia Wazee Tanzania (SAWATA) Mzee Nekemia Mussa Kazimoto, yamefanyika nyumbani katika makaburi ya Nyumbani kwao Kayanga Karagwe mnamo Tarehe 23 Desemba 2019 yakihudhuliwa na maelfu ya waombolezaji, Viongozi na Wageni kutoka ndani na nje ya Nchi.
Akitoa Salaam za rambi rambi Kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (MB) amemuelezea Marehemu Nekemia kama Mzee aliyependa kujituma na kuchapa kazi kwa bidii, na hivyo akiwasihi wananchi kujifunza kupitia kifo cha Marehemu Kazimoto, kuacha alama ya kukumbukwa.
Marehemu Kazimoto ambaye amefariki akiwa na Umri wa miaka 82, kutokana na shinikizo la Damu, pamoja na mambo mengine aliyoyafanya katika enzi za uhai wake, atakumbukwa kama Mzee mwenye hekima na busara kwani amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa nchini ndani ikiwemo kuasisi na kuongoza kupigania haki na stahili za wazee wenzake hapa Nchini kupitia Shirika la Saidia Wazee Tanzania (SAWATA), na huku akitumia uwezo na weledi wake kupigania masilahi ya Wazee.
Marehemu ameacha Mjane mmoja na watoto 14, ambao wapo katika nafasi mbalimbali, huku maisha yake akiwa ameyaweka wazi katika Kitabu alichokiandika Mwenyewe kiitwacho “Maisha na Harakati za Kazimoto” kilichohaririwa na Mzee Mwenzake Pius Ngeze.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rvWtkL
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33
















