π *Ni kupitia fursa za Ajira, Kilimo, Biashara, Afya*
π *Halmashauri ya Muheza yaeleza inavyonufaika na fidia; ushuru wa huduma*
π *Mradi wafikia asilimia 45.5*
Wananchi kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaozunguka Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalojengwa kutoka Uganda mpaka Chogoleani mkoani Tanga, Tanzania wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa mradi huo ambao umeibua fursa mbalimbali ikiwemo za ajira, biashara, kilimo, maji, utunzaji wa Mazingira na umeme.
Wananchi hao wameeleza hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Mradi wa EACOP katika maeneo mbalimbali nchini iliyojumuisha Waandishi wa Habari na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Mradi huo umewanufaisha baadhi ya wakazi katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singinda, Dodoma, Manyara na Tanga ambapo bomba la mafuta linapita huku Watanzania 7,584 wakipata ajira za muda mfupi na muda mrefu.
“Mradi huu wa EACOP umeajiri makundi mbalimbali ya watu ikiwemo Wanawake wanaoishi eneo la mradi ili kuwawezesha kiuchumi, kubadilishana uzoefu na kukuza ujuzi wa Vijana wanaofanya kazi katika kambi mbalimbali nchini,”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza, Dkt. Juma Mhiza ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao umefikia asilimia 45.5 na kueleza kuwa ni chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Muheza na maeneo mengine nchini.
Amesema mradi huo ni fursa kwa Wananchi wa Muheza kwani umeongeza mzunguko wa fedha kwenye jamii ambapo Sh. bilioni 5.4 zimelipwa kwenda kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya fidia ya ardhi kwa maeneo yanayopitiwa na mradi.
Amesema mradi umeongeza mapato ya ndani kwa Halmashauri kupitia tozo na ushuru wa huduma kwa wakandarasi wanaohudumia mradi huo.
Dkt. Mhiza amesema mapato hayo yamewezesha Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye mahitaji maalum kuboresha afya za lishe kwa makundi maalum ya watoto ili kuepuka utapiamlo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Afisa Uhusiano wa Jamii kutoka (EACOP), Bi. Anna Samwel amesema mradi huo unashirikiana vyema na jamii kwa kuwajengea uwezo wananchi waliopo karibu na mradi kwa kutoa elimu ikiwemo ya usalama barabarani, afya, utunzaji wa mazingira, uendelezaji wa miradi ya kilimo na shughuli nyingine ikiwemo ulinzi.
Amesema Mradi unakutana mara kwa mara na wanavijiji kupitia vikao vya maendeleo ili kueleza utekelezaji wake na fursa zilizopo kwenye mradi ikiwemo ajira.
Bi. Anna amesema wafanyakazi wazawa walioajiriwa katika mradi wamenufaika kwa kupata kipato na kusomesha watoto, kuboresha makazi, uendelezaji wa shughuli za kilimo na ufugaji kwenye kaya na jamii.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33











