Kada wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Ndg.Fuya Godwin Kimbita amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi ili kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Aidha Ndugu Fuya aliyefika ofisi za CCM Hai majira ya saa mbili kamili asubuhi juzi jumamosi 28/06/2025 ambapo baada ya Kuchukua Fomu hiyo katika ofisi ya CCM iliyopo Bomang’ombe Wilayani Hai amesema amefurahi na anamshukuru sana Mungu kumfikisha siku ya leo kwani yeye na wana Hai wameisubiri siku hiyo kwa Hamu kubwa.
Kimbita amesema Mbunge aliyopo Madarakani Mhe.Saashisha Mafuwe kwa nafasi yake amefanya kazi nzuri na sasa ni muda wa kuwaacha wengine wamsaidie kwani bado zipo kazi alizozianza tangu 2020 hazijakamilika ila yeye ndiye mwenye mwarobaini wa kuzikamilisha kama alivyofanya 2005 hadi 2010 akiwa mbunge kipindi cha serikali ya awamu ya 4.
Mbali na kuwa mwanachama mwaminifu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Fuya amewahi kuwa mbunge wa Hai 2005 hadi 2010, mjumbe wa Halmshauri kuu (NEC) ya CCM,Mjumbe wa kamati mbalimbali za Bunge,Mjumbe wa kamati za kusaidia Maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi ikiwepo kuwa Mwasisi wa haraambee ya umaliziaji wa ujenzi wa Ofisi ya CCM wilayani hai.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






