Fatma Karume na Kigwangalla Wamekuwa Gumzo Mitandaoni

7 years ago99 Views

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume wamekutana leo kwenye ‘Brunch date’ na kujadili jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya viongozi wanaowasiliana kwa kutumia mitandao.

Baada ya mkutano huo ambao umedumu kwa zaidi ya masaa kadhaa ukianza majira ya saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni, umemalizika kwa wawili hao kuonekana wakifurahia na kuonesha umoja tofauti na jinsi ambavyo huwa wanacharuana mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Kigwangalla amesema mambo yote yamewekwa kando huku akisifu kuwa Fatma maarufu Shangazi ni mtulivu na msikivu sana.

 Shangazi ni mtu poa sana, mnyenyekevu, mvumilivu, msikivu, mwenye uelewa mpana sana wa mambo, na ana sababu zake kwenye kila analofanya. Tungeweza kuongea mpaka asubuhi kwa jinsi mada zilivyokuwa nyingi, nzito na ndefu. Kwa hakika tutakutana tena. Inshaallah

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2FvgWe5
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.