
Kim Porter (47), aliyekuwa mzazi mwenzake rapa maarufu wa Marekani, P Diddy, atazikwa mahali alipokulia, na Diddy amesema atahakikisha anampa maziko yanayomfaa mwanamke huyo ambaye alikuwa ni kipenzi cha roho yake.
Habari zilizopo zinasema Kim atazikwa Jumamosi hii huko Columbus, Georgia, ambako alikulia na kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu mwaka 1988. Ni huko pia mama yake, Sarah, alizikwa mwaka 2014.
Nyumbani kwa P Diddy wakati wa ibada maalum kwa Kim.
Ijumaa usiku wiki hii marafiki na familia ya Kim watakutana kwa chakula cha usiku kabla ya mazishi yake.
Taarifa zinaongeza kwamba jeneza la Kim litakokotwa na farasi na Mchungaji maarufu T.D. Jakes ataendesha ibada ya kumwombea marehemu.
Jumapili iliyopita Diddy alifanya ibada ya kumbukumbu kwa ajili ya Kim nyumbani kwake Bel Air ambako watu wapatao 100 walihudhuria, ikiwa ni pamoja na mastaa kama Montana, Mary J. Blige na Pharrell.
Kim, Diddy.
Porter alikuwa amefariki nyumbani kwake huko Los Angeles Alhamisi iliyopita akidaiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na mafua (flu).
Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo flu ndicho chanzo halisi cha kifo chake. Kim alikuwa ametembelea Afrika muda mfupi kabla ya kifo chake na madaktari wanahisi labda aliambukizwa ugonjwa fulani katika safari hiyo.
Sababu ya kifo chake itatolewa, kwa mujibu wa uchunguzi, baada ya wiki nne hadi sita vijazo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






